Mkuu mkoa wa Tanga, Martine Shigela amefunga mpaka wa Horohoro unaopakana na nchi ya Kenya na Tanzania mkoani Tanga baada ya wakenya 19 kugundulika kuwa na virusi vya Corona.

Wakiwa katika harakati ya kuingia nchi huku hali ya maambukizi ya Ugonjwa huo nchini Tanzania ikiripotiwa kuwa inapungua.

Zikiwa zimepita siku chache tangu madereva wa Watanzania kuzuiliwa mpakani Horohoro wasiingie nchini Kenya kwa kile kinachodaiwa kuwa wapimwe virusi vya Corona na majibu hupatikani ndani ya siku tatu hali iliyopelekea kuharibika kwa bidhaa na madereva kukosa gharama za kujikimu.

Leo mkuu wa mkoa wa Tanga amejibu mapigo kwa kumtaka kamanda wa polisi mkoa wa Tanga kuhakikisha Wakenya hawapenyezi kuingia nchini kwa kulinda mpaka huo usiku na mchana huku wafanyabiashara was mataifa mengine Wakiwa huru kuendelea kupita.

 

The post RC Tanga “Magari yanayotoka Kenya yazuiliwe yasiingie Tanzania, Madereva wao 19 wamekutwa na Corona” – Video appeared first on Bongo5.com.