Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza Punguzo kubwa la Bei ya Nguo la hadi 80% kwenye Maduka Makubwa ya Nguo yaliyopo Jijini humo ili kuhakikisha Wananchi wanapendeza na kuwa nadhifu Jumapili ya May 24 kwenye Kilele cha Siku Tatu za Shukrani Kwa Mungu zilizotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli.

RC Makonda amesema atafurahi kuona kila mwananchi wa mkoa huo anasheherekea kwa nderemo na vifijo siku ya jumapili kama sehemu ya shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Corona na baada ya hapo kila mmoja achape kazi ili kwa pamoja tuinue Uchumi wa Taifa.

Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza Shindano la DJ bora ambapo kila DJ atatakiwa kumtumia Video Clip huku akiwaelekeza wenye Bar, Hotel, Lodge, Band na Biashara kuzifungua.