Marekani imesema huenda Rais Trump na Makamu wake Mike Pence wakalazimika kupima tena corona kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia Mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Katibu wa Habari) kuugua corona, juzi Viongozi hao walipimwa corona baada ya Mfanyakazi wa Ikulu kuugua corona.

Trump mwenyewe ndiye  aliyetangaza siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na wabunge na maseneta kutoka chama cha Republican kwamba Katie Miller, mke wa mshauri wake wa katika masuala ya uhamiaji, Stephen Miller, ambaye pia ni Msemaji wa Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameathirika. 

Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 80,000.