Rais Dkt John Magufuli ametoa wito kwa waajiri kutotumia ugonjwa wa Corona kama kigezo cha kuwanyanyasa wafanyakazi.
Katika salamu zake kwa Wafanyakazi katika siku hii ya Mei Mosi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi katika ujenzi wa Taifa na itaendelea kusimamia maslahi yao na kuboresha mazingira yao ya kazi.
Mwaka huu sherehe hazitafanyika ili kuepusha mikusanyiko ya watu ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Salamu za Mei Mosi. pic.twitter.com/z3C17xNs86
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) May 1, 2020
The post Rais Magufuli salamu za Mei Mosi ” Tuchape kazi Ugonjwa usiturudishe nyuma” appeared first on Bongo5.com.