Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini imepungua ambapo Hospitali ya Amana imebaki na wagonjwa 12, Mloganzila 6, Kibaha wamebaki 22, Aga Khan 31, Hindumandal 16, Regency 17, TMJ 7, Rabinisia 14.

Rais Dkt Magufuli amesema kuwa hata mwanae alipata Corona alijifungia kwenye chumba akaanza kujifukizia, akanywa malimao na Tangawizi na kwa sasa yuko mzima na huo ndiyo ukweli.

The post Rais Magufuli: Idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua, mtoto wangu alikuwa na Corona amepona, chapeni kazi (+Video)  appeared first on Bongo5.com.