Rais John Magufuli amesema anamshukuru Mungu kwa kujibu maombi katika pindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Corona kwani ameuona mkono wake.

“Ameniagiza tena kwenu maneno aliyoyasema kutoka katika kitabu cha pili kutoka kitabu ya mambo ya nyakati 7:13. Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yakasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi kwa niaba ya Rais Magufuli.

Amesama Rais amemuagiza awajulishe waumini na watanzania wote kwamba anashukuru kwa jinsi walivyoitikia wito wa awali wa kutenga siku tatu za kuomba na sasa ni mahali pa kutoa shukrani kwa Mungu.

“Rais amesema ameuona mkono wa Mungu, Rais anasema ameuona miujiza ya Mungu, Rais anasema ameuona upendo wa Mungu na ameyaona maajabu yake kwa watu wake,”.

Aliongezea kusema kuwa “Rais mesema inawezekana yeye asijue kusali lakini anaamini kwa sala za Watanzania wote waliopiga magoti Mungu amewasikiliza na yeye kwetu kwa unyenyekevu mkubwa anasema asante sana Mungu wangu nauhimidiwe na ushukuriwe na uonekane kati ya mataifa yote,”.