Raia wa Italia Silvia Romano aliyetekwa nyara nchini Kenya miezi 18 iliyopita ameachiliwa huru.

Akizungumza kupitia shirika la habari la serikali, RAI, waziri wa mambo ya nje wa Italia Luigi Di Maio amesema kuwa Romano alipatikana nchini Somalia.

Di Maio amesema kuwa Romano anatarajiwa kuwasili mjini Rome leo Jumapili kwa ndege maalum.
Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu kuachiliwa kwake japo gazeti la Corriere della Sera limeripoti kuwa Italia ililipa kikomboleo ili aachiliwe.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte ameshukuru vikosi vya ujasusi vya nje kwa usaidizi wao kwa kupatikana kwa Romano.
Maafisa nchini Kenya hawajatoa tamko lolote kuhusu kuachiliwa Mtaliano huyo. Mnamo Novemba mwaka 2018, watu waliokuwa wenye silaha walimteka nyara Romano aliyekuwa akifanya kazi na shirika la misaada la Africa Milele.

The post Raia wa Italia aliyetekwa nyara Kenya aachiliwa huru  appeared first on Bongo5.com.