Qatar imeanza kutekeleza adhabu mpya ya kifungo cha hadi miaka 3 jela au faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 127, kwa watu watakaoshindwa kutii agizo la kuvaa Barakoa katika sehemu zenye mikusanyiko.

Hatua hiyo, imeanza kufanyiwa kazi huku Misikiti, shule na migahawa ikifungwa ili kukabiliana na ugonjwa wa COVID19 ambao hivi sasa umekuwa ni changamoto kubwa duniani kote.

Adhabu hizi hazitawahusu Madereva watakaokutwa wakiendesha magari huku wakiwa peke yao ndani ya gari.

Mpaka sasa chini ya Qatar ina visa vya Corona zaidi ya 32,600, vifo vilivyotokea ni 15 na Wagonjwa waliopona ni 3,356.

The post Qatar yatekeleza adhabu ya miaka 3 jela au faini ya tsh milioni 127 kwa wasiovaa barakoa appeared first on Bongo5.com.