“Tumerudi kutoka Madagascar jana usiku ila hatujaja na dawa ya kuanza kugawa leo, tumekuja na dawa za kuanza utafiti na uchambuzi maabara, nimepokea simu nyingi, meseji WhatsApp Watu wanataka niwagaie, jamani sina dawa, sijaja na chupa za dawa”- Waziri Kabudi.

“Chupa tumepewa mbili tu (control) ambazo zitasaidia pale Wataalamu watakapochanganya dawa na kufanya utafiti na uchambuzi ili waone kama wamepatia, tumepewa wastani wa box 3 za dawa itakayotumika kama tiba na Box 8 za dawa itakayotumika kama kinga pale utafiti ukikamilika”-Waziri Kabudi.

“Madagascar wameijaribu wakajiridhisha kwamba ni salama ndio maana wanaitumia lakini sisi lazima tuifanyie utafiti na tujiridhishe kuwa inafaa,Ndege ya Rais haiwezi kuja na mzigo wa kutosha kugaiwa kwa Watanzania wote,Nchi yoyote ikituita kwamba ina dawa tutaenda kuchukua”

The post Prf Kabudi: “Dawa hizi za Corona sio za kugawa ni kwa ajili ya utafiti na uchambuzi maabara” appeared first on Bongo5.com.