Nyota wa Manchester City na England, Kyle Walker ametoa maelezo juu ya sababu zilizompelekea kuvunja sheria ya lockdown zaidi ya mara tatu ndani ya saa 24 pekee wiki hii na kumfanya kuingia kwenye matatizo baina yake na klabu wakati tayari alishavunja kanuni hizo za timu wiki chache zilizopita.

The Sun liliripoti kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, wiki chache zilizopita alivunja miongozo ya serikali dhidi ya janga la virusi vya corona baada ya kufanya ‘party’ na hatimaye kuomba radhi.

Lakini pia Walker, amelaumiwa moja kwa kusafiri kwenda nyumbani kwa dada yake huko Prestbury, Cheshire kwaajili ya ‘party’ lakini la pili kuwatembelea wazazi wake waliopo Sheffield kitendo ambacho hakikubaliki ndani ya klabu kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa janga la Corona.

Ukiachiambali safari hizo tatu, siku iliyofuata akiripotiwa kuonekana akizunguka na baiskeli akiwa na marafiki zake katika makazi yake aliyopanga huko Hale.

Walker aliamua kutoa taarifa kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi usiku baada ya taarifa zake kuenea, ambapo alianza kwakusema kuwa anadhani alikaa kimya kwa muda.

”Ninahisi kana kwamba nimekaa kimya kwa muda wa kutosha, kwa kufuatia habari nyingi zilizoandikwa kuhusu mimi na familia yangu. Ninahisi kama sina chaguo ila kuweka mambo hadharani.”

”Nimepitia moja kati ya kipindi kigumu sana katika maisha yangu, ambapo nilibeba majukumu kamili, ila kwa sasa naona kanakwamba ninanyanyasika.”

”Hili sio tu linaniathiri mimi bali linaathiri afya ya familia yangu, lakini pia na watoto wangu. Kuhusiana na matukio ya siku ya Jumatano, nilisafiri kwenda Sheffield kwaajili ya kumpatia dada yangu kadi ya siku yake ya kuzaliwa, lakini pia kuzungumza na watu wachache ambao ninawaamini katika maisha yangu, mlitaka nimtelekeze ?.”

”Nilisafiri kwenda nyumbani kwa wazazi wangu kwaajili ya kuwapelekea chakula, narudia tena wamepitia kipindi kigumu miezi michache iliyopita.”

”Kitu gani wazazi wangu na dada yangu wamefanya mpaka wakastahili maisha yao binafsi kuwekwa hadharani, na picha au kisa mimi kuwafuata nyumbani kwao ?”

Katika taarifa yake ndefu Walker amesema kuwa anahisi kufuatiliwa kiasi kwamba anashindwa hata kuhisi kuwa yupo salama nyumbani kwake mwenyewe na kumalizia kwa kusema kuwa anatambuwa wapo watu watakao kasirishwa na maelezo yake lakini kumekuwa na haja ya watu kufahamu kuhusu maisha yake.

The post Party, baiskeli na uzururaji vyamponza nyota wa Man City appeared first on Bongo5.com.