Meneja Mkuu wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana  

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imefanya maboresho makubwa katika tovuti yao ya kubashiri, ambayo kwa sasa itawawezesha wateja wao na watanzania kiujumla wanaopenda kubashiri kujumuika pamoja.

Wateja wa Parimatch watacheza kwa pamoja michezo yote ya Simulated Reality League, E-Sports, masumbwi na soka ambayo inatarajiwa kurejea Mei 16 ikianza na Ligi ya Ujerumani ‘Bundesliga,’ kwa  kutumia intaneti kidogo.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana  wakati alipokuwa akizundua rasmi jukwaa hilo la kubashiri mtandaoni kupitia www.parimatch.co.tz na kusema kwamba imekuwa ni desturi yao kusikiliza maoni ya wateja wao kila mara na kuamua kuyafanyia uamuzi ili kusudi waweze kuwapatia kitu kilichokuwa bora wateja wao ambao hutumia muda wao ziada kujiburudisha akili zao na Parimatch.

“Tumefanya mabadiliko mazuri, tumerekebisha mambo mengi. Katika kipindi hiki ambapo watu wengi wapo nyumbani tumeona ni vyema kuwapa njia mbadala ya kupata burudani, kukaa ndani ni suala jema lakini pia kwa afya ya akili burudani ina nafasi yake. Wateja wetu wote watatumia taarifa zao za zamani kuingia www.parimatch.co.tz na wataiona Platform yetu mpya. 

Aidha, Maligana amesema katika maboresho hayo ambayo Parimatch imefanya katika kipindi hiki, yataweza kuwaruhusu watumiaji wa simu za android kuitumia kwa njia ya application kwa urahisi na ufanisi mkubwa zaidi.

Pamoja na hayo, Maligana pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kukuburudisha na kusisimua katika kipindi hiki cha Corona na hususani tukisubiri ligi nyingine zirejee.
Kwa upande mwingine.

Parimatch imeendelea kuwa mkombozi mkubwa kwenye soko la michezo ya kubahatisha ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania, kwa kuweza kutoa betting zenye ubora, malipo ya papo hapo kwa haraka baada tu ya mchezo kumalizika bila ya kusahau huduma ya wateja bora ndani ya masaa 24 siku 7 za wiki kwa takribani miaka 25 hadi hivi sasa.