Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ametoa wito wa kuwepo ushirikiano mpana wa kimataifa katika kutafuta tiba na chanjo ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Kupitia ujumbe wake wa siku ya kuenzi sifa za Bikira Maria, Papa Francis amesema ni muhimu kuunganisha nguvu za kisayansi kutafuta chanjo na tiba katika mazingira ya uwazi yanayowezesha kila mtu duniani kupata matibabu yanayohitajika.
Papa Francis amesisitiza mwenendo huo utawezesha ulimwengu kukabiliana na mzozo wa Corona kupitia njia sahihi na madhubuti. Ujumbe wa Papa Francis umetolewa siku moja kabla ya kufanyika mkutano wa kimataifa uloitishwa na Umoja wa Ulaya unaolenga kukusanya kiasi dola blioni 8.2 kusaidia upimaji, matibabu na chanjo dhidi ya virusi vya corona.
The post Papa Francis: Ni muhimu kuunganisha nguvu kutafuta tiba ya COVID-19 appeared first on Bongo5.com.