Nchi za Rwanda na Nigeria kuanzia leo Jumatatu zimeanza kulegeza masharti ya amri ya kusalia ndani kwa wananchi wake kama sehemu ya mapambano dhidi ya corona.

Nigerians cautious as coronavirus lockdown eased - BBC News

 

Nchini Rwanda marufuku hiyo ilikuwa imewekwa nchi nzima, huku Nigeria marufuku hiyo ilihusisha ndani katika mji mkuu wa Abuja, na mji mkubwa kabisa wa Lagos, katika jaribio la kupunguza athari ya kiuchumi barani Afrika.

Nchi hizo mbili, zinaungana na mataifa mengine ya Afrika kama Ghana, Afrika Kusini na Kenya ambayo pia yamelegeza baadhi ya masharti makali ya hatua hizo za watu kusalia ndani.

Mataifa kadhaa ya Afrika yamechukua hatua ya kuweka marufuku hiyo toka mlipuko wa virusi hivyo kuingia barani na kuonesha hatari ya maambukizi ya ndani ya jamii.

Uganda pia inatarajiwa kutangaza kulegeza masharti kesho. Raisi Museveni anatarajiwa kulihutubia taifa hilo jioni ya leo.

Baadhi ya shughuli za kibiashara zinatarajiwa kufunguliwa japo shule zinatarajiwa kuendelea kufungwa mpaka hapo itakapotangazwa.

Japo hatari ya virusi ingalipo, nchi za Afrika zinalegeza masharti na kuonekana kukabiliana vyema na virusi.

Maisha yarejea katika hali ya kawaida RwandaMabasi kubeba idadi nusu ya idadi ya awali

Mabasi kubeba idadi nusu ya idadi ya awali Rwanda

Baada ya siku 45 za kusalia ndani mjini kigali, kulikuwa na shughuli nyingi hii leo, Raia wa Rwanda walirejelelea shughuli zao kwa masharti ya kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Serikali imelegeza masharti iliyochukua kwa misingi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba kuanzia Jumatatu 04/05/2020, baadhi ya watu wataruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kawaida, huku baadhi zikiendelea kufungwa.

Taarifa ilisema kuanzia Jumatatu wakaazi wataruhusiwa kufanya kai zao lakini hawataruhusiwa kuondoka majumbani kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na moja asubuhi.

Rwanda

Biashara za umma na kibinafsi pia zitafunguliwa tena, masoko yatafunguliwa tena lakini ni asilimia 50 pekee ya wafanyabiashara ndio watakaofanyakazi.

Migahawa na hoteli zitaanza kufanyakazi na kufungwa kuanzia saa moja usiku. Aidha, wanariadha wataruhusiwa kufanya mazoezi lakini michezo mengine mikubwa na majumba mengine ya burudani yataendelea kufungwa.

The post Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown appeared first on Bongo5.com.