Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, raia wa Nigeria atarejea klabu hiyo baada ya kuchezea Manchester United kwa mkopo kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya China ambayo imepangiwa kuanza mwezi Julai. (Sky Sports)

Odion Ighalo

Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, atarejea klabu hiyo kutoka Manchester United

Huku hayo yakijiri, Manchester United wamefufua malengo yao ya kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Sport, via Mail)

Tottenham na Arsenal wameongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa sababu mashauriano ya kiungo huyo wa miaka 31 kurefusha mkataba Chelsea yamegonga mwamba. (football.london)

ChelseaWachezaji wa Chelsea wakisherehekea ufungaji bao

Borussia Dortmund wanataka kumsaini kinda wa Chelsea ambaye anacheza safi ya kati Charlie Webster 16, na kumpandisha hadhi hadi kiwango cha Jadon Sancho. (Sun)

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amekiri kwamba itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuwapoteza wachezaji wake nyota msimu huu – licha ya tetesi kuwa Chelsea inamnyatia mshambuliaji Ufaransa wa miaka 23-Moussa Dembele. (Star)Moussa DembeleChelsea inamnyatia mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele

Baba yake kiungo wa kati wa Brazil Gerson, amedai kuwa Arsenal na Tottenham wanapania kumsaini mchezaji huyo wa miaka 22 kutoka Flamengo. (ESPN, in Portuguese)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kumfuatilia Dries Mertens, ripoti zinasema Lampard amewasiliana moja kwa moja na mashambuliaji huyo wa miaka 33- wa Ubelgiji na Napoli. (Express)Dries MertensDries MertenSs amefungia Napoli mabao 116

Manchester City inataka kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain Edouard Michut, 17. (Sky Sports)

The post Ni vita ya fedha Tottenham dhidi ya Arsenal kuwania saini ya Willian, wengine sokoni appeared first on Bongo5.com.