Ndege ya Shirika la kimataifa la ndege la Pakistani -Pakistan International imeanguka katika mji wa Karachi lipokua ikitoka Lahore, maafisa wa safari za anga wamesema.

Ndege hiyo Chapa PK8303, ambayo ilikua imewabeba abiria 91 na wahudumu wa ndege wanane, ilikua ikisafiri kutoka Lahore kuelekea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah wenye shuguli nyingi zaidi nchini Pakistan.

Waziri wa afya wa jimbo amethibitisha vifo vya watu 11, lakini inahofiwa kuwa idadi ya vifo itaongezeka na kuwa ya juu zaidi.