Kundi la muziki wa Bongo Fleva linaloundwa na wasanii wawili ambao ni Nahreel na Aika ambao pia wako kwenye mahusiano la Navy Kenzo wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya, ya pili miaka mitatu badaae baada ya AIM (Above Inna Minute) iliyotoka mwaka 2017.

Hitmakers hao wa nyimbo kama KATIKA, KAMATIA, GAME na FELLA wamekuwa  kimya kwa muda huku wakiachia kazi moja moja bila mashabiki wao kujua mipango yao kimuziki imekaaje, lakini hivi karibuni watu waliokaribu na wasanii hao wamesema kuna mengi mazuri ya kutegemea kutoka kundi hilo kwani wapo njiani  kuachia album yao mpya itakayoonyesha madiliko waliyoyafanya  kipindi chote cha ukimya wao. “Wamekuwa wakishinda studio sana na muda mwingi wamekuwa wakiutumia kurekodi kazi zao mpya.

Awali ilitakiwa watoe EP Project lakini kila wakikaa na kupitia stock yao ya nyimbo wakajikuta inawawia vigumu kufanya maamuzi ya kukamilisha EP hiyo na kuwapa mashabiki project yenye nyimbo chache kwani wanahitaji kitu kikubwa sana kutoka kwao kama fidia ya ukimya wao. Hivyo wazo la kutoa EP kama limewekwa pause kidogo. Sasa hivi nguvu
yao kubwa imewekezwa kwenye kuanda a full-project itakayowaridhisha mashabiki kuwa ukimya wao haukuwa wa
bure…”

Haijawekwa wazi project hiyo itakuwa na nyimbo ngapi au itaitwaje, ila watu walio karibu na kundi hilo wanasema ni project ambayo itakidhi kiu ya muziki wa Navy Kenzo uliokosekana kwa muda kidogo: “Unajua Navy Kenzo sio watu wa kelele nyingi, mara nyingi wao huacha muziki wao ufanye hiyo kazi kwa niaba yao.

Ila kama ni kurekodi, wanarekodi sana au niseme wamekuwa wakirekodi sana. Ukikaa studio pale kwa Nahreel huwezi kukosa ngoma kali. Wana muziki mwingi sana, kila siku wanajaribu kurekodi vitu vipya na ideas tofauti tofauti mpya ili kupata kitu kilichobora. Hii project mpya ni kazi kubwa sana; kuanzia sound ya muziki, production, vibes, na miondoko yake. Wamejitahidi sana Navy Kenzo wanajua.

Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mambo mengi mazuri kwa Navy Kenzo, waliachia nyimbo kadhaa ikiwemo: FELLA yenye views zaidi ya 1,800,000 kwenye mtandao wa YouTube, MAGICAL yenye views zaidi ya 350,000 na ROLL IT yenye views zaidi ya 350,000 pia ambazo kazi zote hizi zilikuwa zina ashiria kuwa kundi hilo linachukua direction mpya ya muziki wao na pengine kulenga zaidi soko la mbele kitendo ambacho pia kiliwapa fursa ya kushiriki katika festival kubwa ya muziki wa Africa; AFRO NATION GHANA ambapo matokeo yake yaliwezesha kundi hilo kutengeneza uhusiano na wasanii wengine wa Africa amabao baadhi yao tunaweza kuwategemea kuwaona kwenye project yao mpya: “Ghana ilikuwa experience kubwa sana kwao, connections walizotengeneza kati yao na wasanii wengine walioenda kushiriki kwenye festival hiyo inaonyesha ni jinsi gani walivyo na nafasi ya kufanya vitu vikubwa sana.

AFRO NATION GHANA haikuwa tu wao kwenda kuperform bali kutengeneza pia opportunity za kushirikiana katika kazi za muziki na wasanii na maproducer wa kule, na imani wachache wao watakuwepo kwenye album. Wamefanya kitu kikubwa sana kwenye hii project. Hii sio tu project ya Navy Kenzo, ni project ya mashabiki, wadau wa muziki na watu wote barani Africa na duniani wanaopenda muziki mzuri, hasa good African music. Endelea kuwafuatilia utaona.”

Hivi karibuni pia Navy Kenzo kupitia Instgram LIVE yao walikuwa na Mzazi Willy Tuva mtangazaji maarufu wa redio kutoka Kenya na katika mazungumzo yao kuchangia ukarabati wa studio ya muziki “8hoodmusic” inayosaidia kuinua Vipaji vya wasanii waishio kwenye hali na mazingira duni iliyopo Kibera, Kenya; kundi hilo liliulizwa juu ya mipango yao kwa huu mwaka na kusema wanajiandaa kutoka project mpya mwezi Juni;

Navy Kenzo binafsi bado hawajaweka wazi kuhusiana na hili; ila waliokaribu na kundi hilo wanasema tukae chonjo na tutegemee project mpya kutoka kundi hilo pendwa la muziki kutoka Tanzania karibuni.

The post Navy Kenzo na ujio wa Album yao ya pili, Waeleza mipango yao na muda wa kuiachia appeared first on Bongo5.com.