Naibu waziri katika serikali ya Uingereza Douglas Ross, amejiuzulu leo kwa kushindwa kwa Waziri Mkuu Boris Johnson kumfuta kazi msaidizi wake wa ngazi ya juu kwa madai ya kukiuka sheria ya watu kutotoka nje zilizowekwa kupambana na virusi vya corona.

Who is Tory MP Douglas Ross? - BBC News

Johnson alimkingia kifua Dominic Cummings kuhusiana na uamuzi wake wa kuendesha gari kilometa 400 kwenda katika nyumba ya wazazi wake mwishoni mwa mwezi Machi, licha ya amri ya kitaifa kwa watu kubakia majumbani mwao.

Cummings anasema alisafiri ili familia yake iweze kumpa matunzo mtoto wake mwenye umri wa miaka minne iwapo yeye pamoja na mkewe, ambao wote walishukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, wataugua.

Lakini Waingereza wengi wanasema Cummings alionesha kejeli kwa hatua za watu walioamua kufuata sheria ili kujitoa muhanga kuzuwia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, hata wakati ilikuwa na maana kukaa mbali na wapendwa wao.

The post Naibu Waziri Uingereza ajiuzulu kisa msaidizi wa Waziri Mkuu kuvunja sheria za lockdown appeared first on Bongo5.com.