Msanii wa Bongo Movie na mtangazaji wa kituo cha Clouds Plus Mwijaku ametoa amoni yake kuhusu mwenendo wa muziki wetu wa Bongo Fleva.

Mwijaku aliotoa maoni yake baada ya miezi kadhaa kutambulishwa wasanii watatu kwa wakati mmoja huku wote wakitoka katika lebo tofauti tofauti, Wasani hao walikuwa ni Tommy Flavour kutoka Kings Music iliyopo chini ya Alikiba, Zuchu kutoka WCB iliyopo chini ya Diamond Platnumz na Ibrah kutoka Konde Gang iliyopo chini ya Harmonize.

Mwijaku alisema kuwa watu waliona jinsi kila mtu alivyokuwa Attention kusikiliza kila nyimbo ya msanii na kutoa maoni yake kuhusu wasanii hao, lakini yote imeletwa na mabifu ambayo yanaendelea kati ya Alikiba na Diamond. Mwijaku aliongeza kuwa anachofurahi bifu lao ni la kazi tu na sio la kulogana ila ingekuwa wanalogana basi asingependa kuona bifu hilo linaendelea.

“Wewe sikilizia ukisikia Diamond anaachia wimbo hata Alikiba huwa Attention kujua wimbo gani unaachia na ukishaachiwa anausikiliza kwanza anaona wa kawaida au laah, pia kwa upande wa Diamond Alikiba akitangaza anaachia wimbo Diamond lazima ausikilize aone je ukoje…..? Hiyo inaleta ladhaa ya muziki lakini ingekuwa hakuna huo utofauti basi kila mtu angekuwa anajiachilia nyimbo tu hakuna attention”

Mwijaku aliongeza kuwa “Mfano mzuri Ommy Dimpoz huwa hashangai sana nyimbo za Alikiba kwa sababu huwa amezisikiliza kabla ya kutoka pia nitolee mfano Wizkid na Davido wao wamemaliza bifu ila hawashirikishani kwenye muziki wananshirikishana kwenye mambo ya kijamii tu ikija suala la muziki kila mmoja anafanya kivyake hiyo ndio inaitwa Attention ya muziki, Simaanishi kwamba wasanii hakuna ila wasanii wengine hawajachangamka kama wao”

“Siku wakipatana Alikiba an Diamond hata ladhaa ya muziki wetu inaishi na muziki wetu utakufa pale pale”

The post Mwijaku: “Siku Diamond na Alikiba wakimaliza bifu muziki wetu siku hiyo hiyo unakufa, Wengine hawajachangamka” – Video appeared first on Bongo5.com.