Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MTUMISHI benki ya Boa, Nahami Mwaipyana, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka saba ya wizi akiwa Mtumishi na shtaka moja la utakatishaji wa fedha wa zaidi ya USD 35 elfu na Tsh. Milioni mbili.
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Mwandamizi Anna Chimpaye amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa mshtakiwa ametenda makosa ya wizi akiwa mtumishi katika tarehe tofauti tofauti kuanzia Januari 2017 hadi Novemba 2018.
Katika shtaka la kwanza imedaiwa, Januari 4, 2018 huko Bank of Africa (BOA) tawi la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam , mshtakiwa aliiba USD 8200 mali ya mwajiri wake.
Mshtakiwa huyo anadaiwa Novemba 29 2017 aliiba USD 10,000 wakati Oktoba 18, 2017 Liiba USD 12,700. Pia Machi 6 2017 aliiba USD 5000 huku Augusti 21 akidaiwa kiba Tsh.milioni moja.
Imeendelea kudaiwa kuwa Novemba 6,2017 mshtakiwa Nahima aliiba Tsh. 970,000 huku Augusti 18,2017 aliiba Tsh. 930,000.
Katika shtaka la utakatishaji fedha imedaiwa kati ya Januari Mosi 2017 na Februari 28,2018 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alitakatisha kiasi cha USD 35900 pamoja na fedha za kitanzania Sh. 2,900,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi akiwa mtumishi.
Hata hivyo, mshtakiwa ameku kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kuwa shtaka la utakatishaji fedha linalomkabili halina dhamana kisheria.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 20,2020 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa mshtakiwa amerudishwa rumande.