Familia moja inayopatikana Kinyanambo A Halmashauri ya mji wa Mafinga mkoani Iringa, imelazimika kuishi katika mazingira magumu na ya hofu baada ya mmoja wa Watoto wa familia hiyo kuwa na nguvu ajabu inayotoa moto unaounguza vitu vya ndani.

Nyumbani kwa familia hiyo

Familia ya Peter Mlomo imejikuta katika wakati mgumu, baada ya kupoteza baadhi ya mali zinazodaiwa kuunguzwa na mmoja wa watoto wa familia hiyo, ambaye anatajwa kuwa na nguvu ya ajabu ambayo hutoa moto unaounguza vitu vya ndani.

Justin James Lyakungi ni mchungaji wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) amemfanyia maombi mara baada ya hali hiyo kujitokeza lakini bado haionekani kusadia.

Mtoto huyo ana umri wa miaka 11, pindi hali hiyo inapomtokea mapigo ya moyo wake huwa  yanakwenda kasi na baadae moto hutokea na kuanza kuunguza vitu vyandani na ajabu ni kwamba moto huo unaunguza vitu vya familia na ndugu zake tu na si vinginevyo.

View this post on Instagram

Mtoto atoa moto wa ajabu unaounguza vitu ndani, Mtoto azungumza haya. Familia moja inayopatikana Kinyanambo A Halmashauri ya mji wa Mafinga mkoani Iringa, imelazimika kuishi katika mazingira magumu na ya hofu baada ya mmoja wa Watoto wa familia hiyo kuwa na nguvu ajabu inayotoa moto unaounguza vitu vya ndani. Familia ya Peter Mlomo imejikuta katika wakati mgumu, baada ya kupoteza baadhi ya mali zinazodaiwa kuunguzwa na mmoja wa watoto wa familia hiyo, ambaye anatajwa kuwa na nguvu ya ajabu ambayo hutoa moto unaounguza vitu vya ndani. Justin James Lyakungi ni mchungaji wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) amemfanyia maombi mara baada ya hali hiyo kujitokeza lakini bado haionekani kusadia. Mtoto huyo ana umri wa miaka 11, pindi hali hiyo inapomtokea mapigo ya moyo wake huwa  yanakwenda kasi na baadae moto hutokea na kuanza kuunguza vitu vyandani na ajabu ni kwamba moto huo unaunguza vitu vya familia na ndugu zake tu na si vinginevyo. (📹 via Eatv) by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Mtoto atoa moto wa ajabu unaounguza vitu ndani, Azungumzia inavyokuwa – Video appeared first on Bongo5.com.