Afisa wa zamani wa ngazi ya juu wa afya nchini Marekani ameliambia bunge la kongresi kuwa nchi inaweza kukabiliwa na “kipindi kibaya zaidi cha majira ya baridi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya hivi karibuni ” kwa sababu ya virusi vya corona.

Rick Bright aliongoza shirika la serikali kujaribu kutengeneza chanjo,lakini akaondolewa katika kazi hiyo mwezi uliopita.

Awali alisema aliondolewa kazini kwa kuelezea hofu juu ya tiba zinazotangazwa na rais Donal Trump.

Rais Trump alimfuta kazi kwa madai kuwa alikua mtumishi “asiyeridhika”

Bwana Bright pia aliiambia kamati ya Bunge la wawakilishi ya masuala ya afya kuwa ”maisha yanapotea” kwa sababu ya serikali “kutochukua hatua ” katika hatua za mwanzo za mlipuko wa virusi vya corona.

Alisema kuwa kwa mara ya kwanza alizungumzia juu ya ukosefu wa zana za matibabu mwezi Januari, na kufikisha suala hilo katika “ngazi za juu” za Wizara ya Afya na huduma za binadamu (HHS), lakini “hakujibiwa”.

Ni nini kingine alichosema Bwana Bright ?

Wakati wa ushahidi, Bwana Bright alionya kwamba ” dirisha ” la kushughulikia virusi vya corona linakaribia “kufunga”.

“Kama tutashindwa kuboresha jinsi tunavyokabiliana na ugonjwa huu sasa, kwa misingi ya sayansi, ninaogopajanga litakua baya sana na kuendelea kwa muda mrefu ,” alisema.

“Bila mpango bora, 2020 unaweza kuwa na kipindi kibaya zaidi cha majira ya baridi kuwahi kushuhudiwa katika histioria ya sasa .”

Bwana Bright pia ameiambia kamati hiyo ya bunge la wawakilishi kuwa mwezi Januari alipokea barua pepe ambayo “hawezi kusahau “, kutoka kwa wasambazaji wa barakoa za hospitali ambao walioonya juu ya upungufu mkubwa wa barakoa,

“Alisema… tunahitaji kuchukua hatua.Na nikaituma barua hiyo kwa ngazi ya juu ya HHS – na sikupata jibu.”

 

Bwana Bright alisema kuwa kuondolewa kwake kazini kulikua ni matokeo ya kuendelea kwake kusisitiza kwamba pesa zilizotengwa na Kongresi za kukpambana na mlipuko wa virusi zinapaswa kuwekwa “katika suluhu salama na zilizochunguzwa kisayansi na sio katika madawa , chanjo au teknolojia nyingine ambazo hazijathibitishwa kisayansi “.

“Nilizungumza wazi wakati ule, na ninatoa ushahidi leo, kwa sababu sayansi sio siasa au upendeleo -lazima iongoze katika njia ya kupambana na virusi,” aliongeza.

Ni kwanini ilikua hatari kuondolewa kwenye wadhfa kwa Rick Bright ?

Malalamiko ya mfichuzi , yaliwasilishwa mapema mwezi huu, yanasema kuwa Bwana Bright aliondolewa kwenye wadhfa wake kama Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kimatibabu – Biomedical Advanced Research and Development Authority (Barda) kwa sababu za kisiasa.

Bwana Bright anasema aliondolewa muda mfupi baada ya taarifa kuhusu chloroquine, ambayo alisema alikuwa chanzo chake.

Rais Trump alikua amesema kuwa hydroxychloroquine, dawa ya malaria ina uwezekano wa “kuleta mabadiliko ” katika tiba ya Covid-19-ingawa wataalmu wengi wamesema kuwa huenda isiwe ya ufanisi, au hata ikawa hatari.

Malalamiko ya Bwana Bright yalikua ni kwamba aliamua kuzungumza na waandishi wa habari kwa sababu maafisa wa serikali “walikataa kusikia ” tahadhari zake.

Alisema alikua na jukumu la kujaribu na kulinda umma “kutoka kwa madawa ambayo anaamini ni ya hatari kwa usalama na afya ya umma”.

Trump alijibu vipi ?

Trump

Baada ya kusikia, Rais Trump aliwaambia waandishi wa habari : “Simfahamu.Sijawahi kukutana nae.Sitaki kukutana nae.”

“Lakini nilimtazama , na anaonekana kama mtu mwenye hasira, mtumishi asiyeaminika , ambaye kusema kweli kwa mujibu wa baadhi ya watu hakufanya kazi nzuri sana .”

Waziri wa afya Alex Azar alidai kuwa maafisa walifuata mapendekezo ya Bwana Bright.

“Kila alichokilalamikia kilifanikiwa-anachokizungumzia kilifanyaka ,” alisema Bwana Azar

“Alisema kuwa alizungumzia kuhusu haja ya kupata vifaa vya kusaidia kuongeza oksijeni kwenye mapafu.Tuliagiza vifaa hivyo(respirators) kutokana na maagizpo ya rais.

Alisema tunahitaji mradi wa Manhattan wa chanjo. Tukawa na Mradi wa Manhattan.”

Jumla ya watu 85,807 wamekufa hadi sasa kutokana na virusi vya corona nchini Marekani . Jimbo la New York linaendelea kuwa na idadi ya juu zaidi ya vifo nchini Marekani, likiwa na vifo 27,607

Chanzo BBC

The post Mtaalamu wa chanjo Marekani: “Kipindi cha baridi kikifika taifa letu litazidiwa na Corona” appeared first on Bongo5.com.