Msichana Darnella Frazier (17) ambaye amerekodi video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Polisi akimkandamiza shingoni George Floyd hadi kufariki,  amesema amepata kiwewe baada ya kurekodi tukio hilo.

Kijana huyo amesema baada ya kupost video mitandaoni ambayo imesambaa Dunia nzima, amepokea ukosoaji mwingi kwa kutoingilia wakati Polisi alipokuwa amekandamiza  goti kwenye shingo ya George Floyd hadi kufariki.

Sijatarajia mtu yeyote aliyekuwa kwenye nafasi yangu kuelewa na ninavyojisikia nilivyofanya tukio lile, mimi ni mchanga nina miaka 17 naogopa kupigana na Polisi kwa sababu walikuwepo pale na kupigana kunaweza mtu mwingine auawe hapohapo, hata nisingekuwa mimi bado Polisi wangefanya kazi yao na ningeenda ningesababisha matatizo mengine” ameeleza msichana Darnella Frazier.

Polisi aliyefanya tukio la mauaji kwa George Floyd na wenzake watatu wamefukuzwa kazi huko Minneapolis nchini Marekani, na baadhi ya watu maarufu na wasanii nchini humo wamepinga vikali na wamekemea tukio hilo na kutaka haki za watu weusi zilindwe.

The post Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe appeared first on Bongo5.com.