Félicien Kabuga, miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, amekamatwa karibu na mji wa Paris, wizara ya sheria ya Ufaransa imetangaza.

Bwana Kabuga ameshikiliwa na polisi mjini Asnières-Sur-Seine, eneo ambalo alikuwa anaishi kwa utambulisho wa uongo.

Mahakama ya kimataifa ya mauji ya kimbari yaliyotokea Rwanda yamemshtaki bwana Kabuga mwenye umri wa miaka 84-kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa wahutu ambao waliuwa watu 800,000 mwaka 1994.

Walikuwa wanawalenga kundi dogo la jamii ya Tutsi pamoja na wapinzani wao siasa.

Marekani ilitoa dau la dola milioni 5 kwa atakayeweza kutoa taarifa kuhusu bwana Kabuga ili aweze kukamatwa.

The post Mshukiwa mkubwa wa mauaji ya Kimbari akamatwa Ufaransa appeared first on Bongo5.com.