Mgombea urais nchini Marekani katika tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amekanusha vikali madai ya kumdhalilisha kingono Tara Reade ambaye alikuwa afisa wake wa zamani, huku akiongeza kuwa kisa hicho ambacho mwathiriwa anadai kilitendeka mwaka 1993, hakikutokea.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha MSNBC, Biden amekivunja kimya chake cha mwezi mmoja kuhusu suala hilo kwa kusema kuwa hajawahi kutenda uhalifu huo.
Aidha, taarifa ya Biden imesema waliokuwa wasaidizi wake wakuu mnamo wakati kisa hicho kinadaiwa kutokea, wamekanusha kufahamu tukio hilo.
Mgombea huyo wa Democrat amesema ataliomba idara ya taifa inayohusika na kuweka rekodi kuchunguza ikiwa kuna rekodi yoyote ya malalamiko hayo. Reade ni miongoni mwa wanawake ambao wamelalamika kwamba Biden aliwabusu na kuwashika kwa njia isiyofaa.
Makamu huyo wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden atakiwakilisha chama cha Demokratic katika kuchuana na na Rais Donald Trump uchaguzi ujao mwezi Novemba.
The post Mpinzani wa Trump uchaguzi ujao wa Rais, Joe Biden akanusha madai ya kumdhalilisha kingono msaidizi wake appeared first on Bongo5.com.