Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amesema kuwa mpaka sasa hakuna dawa yakuzuia au kutibu Corona hivyo amewahasa wananchi kuwacha kutumia baadhi ya dawa ambazo wanadhani zinaweza kutibu ugonjwa huo.

Prof. Abel Makubi amezitaja baadhi ya dawa hizo ambazo kumekuwa na uvumi wa kutibu au kuzuia ugonjwa wa Corona kuwa ni Azithromycin, Aspirin, Prednisolone, Zinc, vitamini C na baadhi ya dawa zakutibu ugonjwa wa Ukimwi (ARV).

“Mpaka sasa hakuna dawa yakuzuia au kutibu Corona ” Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi

 

The post ”Mpaka sasa hakuna dawa yakuzuia au kutibu Corona”- Mganga Mkuu wa Serikali (+Video) appeared first on Bongo5.com.