George Floyd, mmarekani mwenye asili ya Afrika(aliye lala chini) ameuawa kikatili baada ya kukanyagwa shingoni na polisi  'mzungu' huku mwili wake ukiingizwa uvunguni mwa gari.

Floyd aliuawa Jumatatu na  polisi mzungu nchini Marekani katika mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota. 

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Marekani, ilimuonyesha polisi mzungu akiwa amemlaza chini mtu huyo kifudifudi huku akiwa amemkandamiza vibaya shingo yake kwa goti la mguu wa kushoto. 

Mtu huyo mwenye asili ya Afrika aliyejulikana kwa jina la George Floyd alikuwa akipiga kelele kwa kusema: "Umenibana shingo siwezi kupumua" "Naomba maji" na "Usiniue" hadi alipofariki dunia.

Kufuatia ukatili huo , meya wa mji wa Minneapolis, Jacob Frey amewafuta kazi maafisa wanne wa polisi kwa kusababisha kifo cha Floyd.

Vitendo vya ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani weusi, vimekuwa vikiibua maandamano na malalamiko ya raia wa nchi hiyo.