YANGA imeanza mazoezi yake ikiwa chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwasa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria Dar es Salaam.

Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja yupo tayari kuonyesha kile alichonacho kwa ajili ya manufaa ya timu.

"Wachezaji wapo sawa na kila mmoja anafurahi kuwa kwenye mazoezi imani yetu ni kuona kwamba tunatoa burudani uwanjani pale ligi itakapoanza kurindima," amesema.

Kocha Mkuu, Luc Eymael amekwama nchini Ubelgiji kutokana na kufungwa kwa anga la kimataifa la ndege wakati huu wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.