Kufuatia hotuba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania ya tarehe 3 Mei, 2020 wakati akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria, ambapo pia alibainisha changamoto za utendaji wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) amechukua hatua zifuatazo.

  1. Amemwelekeza Katibu Mkuu (Afya) kuwasimamisha kazi mara moja Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii Dkt. Nyambura Moremi na Bwana Jacob Lusekelo Meneja Udhamini wa Ubora ili kupisha uchunguzi.
  2. Mhe. Waziri ameunda kamati ya wataalam wabobezi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mwendeno wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ikiwemo Mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za COVID- 19.

The post Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa, meneja udhiti kusimamishwa kazi, uchunguzi kufanyika  appeared first on Bongo5.com.