Mamlaka za mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul zimeamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya virusi vya corona vinavyoibua wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la kusambaa virusi hivyo hatari.

Meya wa mji huo Park Won-soon amesema amri hiyo itakayoendelea bila kikomo imefuatia maambukizi mapya ya virusi vya corona yaligundulika kwenye wilaya ya Itaewon, yenye shughuli nyingi nyakati za usiku. Zaidi ya visa 24 vinahusishwa na mwanaume mmoja aliyegundulika kuwa maambukizi ya COVID-19 baada ya kutembelea kumbi tano za starehe kwenye wilaya ya Itaewon wiki iliyopita.
Korea Kusini imekuwa mfano kwa jinsi ulimwengu unavyoweza kukabiliana na virusi vya corona, lakini meya wa mji wa Seoul ameonya uzembe unaweza kusababisha wimbi jipya la maambukizi
The post Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona appeared first on Bongo5.com.