Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii zinazosema kuwa watu 92 wamekufa mkoani Morogoro kwa corona katika kipindi cha wiki moja na kuzikwa kwenye makaburi ya Kola yaliyopo katika manispaa ya Morogoro.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mkoani hapa mara baada ya kutembelea eneo hilo la makaburi na kufanya uchunguzi wa kuyaona makaburi hayo kama yanayotangazwa.
“Kumekuwepo na taarifa zinazoashiria matumizi yasiyo sahihi ya kimtandao na hivyo kuleta taharuki kwa wakati wa Morogoro,nimefika hapa nijionee mwenyewe makaburi hayo 92,sijayaona hayo makaburi yaliyosemwa”.Alisema Prof. Makubi.
Hata hivyo Prof. Makubi alisema hakuna maziko ya usiku yanayofanyika kwenye makaburi hayo,kauli hiyo ilisisitizwa pia na mtunzaji wa makaburi hayo ALLY KASOLE ambaye alisema maneno hayo ni uvumi.
Prof. Makubi amewatahadharisha ndugu wa marehemu kuacha fungua miili iliyokwisha kufungwa na wataalamu wa afya.
The post Mganga Mkuu Morogoro “Hakuna watu 92 waliokufa kwa Corona” appeared first on Bongo5.com.