Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi April,2020 umepungua hadi asilimia 3.3 %kutoka asilimia 3.4% kwa mwakaulioishia Machi 2020.
Hayo yamesemwa juzi jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na takwimu za Jamii Bi Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa hii inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwakaulioishia mwezi April ,2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi Machi ,2020.
Kupungua kwa mfumuko wa bei ulioishia kwa mwaka ulioishia April,2020 kumechangiwa kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia n Mwezi April ,2020 ikilinganishwa na bidhaa za mwezi April,2019.
Aidha,Bi Minja ameainisha baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi April,2020 ikilinganishwa na mwezi April,2019 kuwa ni pamoja na unga wa ngano kwa asilimia 1.4%,matunda kwa asilimia 6.8%,viazi vitamu kwa asilimia 5.5%,na ndizi za kupika kwa asilimia 7.9%.
Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi April,2020 ikilinganishwa na bei za Mwezi April,2019 ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 4.6%,dizeli kwa asilimia 7.2% na petrol kwa asilimia 3.8%.
Pia Bi.Minja ameainisha baadhi ya vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi April 2020 u umepungua hadi asilimia 4.6% kutoka asilimia 5.3%kwa mwaka ulioishia mwaka ulioishia mwezi kwa mwaka ulioishia mwezi Machi ,2020.
Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ,nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwaka ulioishia mwezi April 2020 umeongezeka hadi asilimia 5.62% kutoka asilimia 5.51% kwa mwaka ulioishia Mwezi Machi,2020 na nchini Uganda umeongezeka asilimia3.2% kutoka asilimia 3.0%.
MWISHO.