Wakati baadhi ya makocha na mabeki wakiweka wazi kuwa ubora wa Meddie Kagere unawasumbua, mshambuliaji huyo Mnyarwanda ameweka wazi mambo matano anayoyafanya katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona (COVID 19).

Kagere alisema ratiba yake ya siku inaanza kwa kushiriki ibada ya kufunga, kuswali na kipengele chake namba tatu ni kufanya mazoezi ya viungo kwa lengo la kujiimarisha na kujiweka tayari kwa kumalizika msimu wa 2019/20.

Kwa mujibu wa NIPASHE, Mshambuliaji huyo alisema baada ya hapo programu yake inayofuata ni kuangalia filamu na humaliza na kitendo cha kupumzisha mwili wake kwa kulala.

“Ninafanya kile ambacho nimepanga, hii ni kuniandaa na ligi ambayo bado msimu haujamalizika,” alisema kinara huyo wa mabao msimu huu na mshindi wa Tuzo ya Mfungaji Bora msimu uliopita.

Mrundi Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo aliliambia gazeti la NIPASHE kuwa Kagere ni mmoja wa washambuliaji hatari ndani ya Ligi Kuu Bara.

The post Meddie Kagere aanika mambo matano anayofanya kipindi hiki appeared first on Bongo5.com.