Mchezaji wa klabu ya Tottenham Son Heung-min ,27, amemaliza jeshi kwa mujibu wa sheria za nchi yake ya Korea Kusini, Ikumbukwe kila kijana wa taifa hilo kuanzia umri wa miaka 18 – 28 lazima kwenda jeshini kwa miezi 21.

Kilichopelelea Son kwenda kwenye mafunzo kwa muda mchche ni kutokana na kuisadia timu yake ya taifa ya Korea Kusini kutwaa Asian Game 2018.

Inaelezwa Son ametunukiwa tuzo ya utendaji bora wa kazi kwa kujituma kati ya wenzake 157.

Mmoja ya viongozi katika serikali ya Jamuhuri ya Korea Marine Corps aliiambia Korea Herald kuwa “Son alipokea tuzo ya ‘Pilsung’ ambayo ni moja wapo ya aina tano ya tuzo za Utendaji bora.

The post Mchezaji wa Tottenham Son, Amaliza mafunzo ya Kijeshi na kutunukiwa tuzo ya Utendaji bora appeared first on Bongo5.com.