Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani humo Suleiman Masoud Suleiman Maarufu Suleimwn Nchambi kwa tuhuma za kupatikana na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali.

Kwa mujibu wa Clouds media. Kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga ACP, Debora Magiligimba amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa Mei, 3 nyumbani kwake Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga baada ya kikosi kazi cha kiintelejensia kupata taarifa za siri kuwa Mbunge huyo amekuwa akijihusisha na uwindaji haramu ambapo katika uchunguzi silaha 6 anamiliki kihalali na 10 hazina vibali vya umiliki.

Silaha aina mbalimbali zimekamatwa katika makazi ya mbunge huyo ikiwemo Shortgun 1, na aina zingine 15, kilo za nyama 35 zinazodhaniwa kuwa ni za wanyamapori ambazo sampuli zake zimepelekwa kwa mkemia mkuu.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

The post Mbunge CCM akamatwa na Polisi baada ya kukutwa na silaha 16 na risasi 536 appeared first on Bongo5.com.