Kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo cha John Hopkins, takriban visa vipya 18,873 na vifo 808 vimerekodiwa jana, Mei 17 2020.

Hivi sasa Marekani ina jumla ya visa 1,674,644, wagonjwa waliopona ni 313,809 huku waliofariki dunia wakiwa 92,639.

Bado Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi na mlipuko wa COVID19. Mataifa mengine yenye idadi kubwa ya maambukizi ni pamoja na Urusi, Uhispania, Uingereza na Brazil.

Ulimwenguni kote, visa viliyorekodiwa ni 4,743,780, waliopona ni 1,698,902 na waliopoteza maisha ni 314,785.

The post Marekani yarekodi visa vipya 18000 vya corona appeared first on Bongo5.com.