Marekani imeidhinisha majaribio ya dawa ya dharura kutumika kwa wagonjwa wenye virusi vya corona, wakati majimbo zaidi nchini humo yakilegeza masharti ya kutotoka nje licha ya vifo vitokanavyo na virusi hivyo kuzidi kuongezeka.

FDA allows emergency use of Remdesivir for coronavirus

Kuidhinishwa kwa dawa hiyo ni hatua ya hivi karibuni ya juhudi za dunia kupata tiba kamili na chanjo ya virusi vya corona vilivyowaacha nusu ya watu duniani wakibakia nyumbani, kuutikisa uchumi wa dunia na kuwaambukiza watu zaidi ya milioni 3.3 ulimwenguni.

Dawa hiyo inayojulikana kama Remdesivir, iliyotengenezwa kupambana na ugonjwa wa ebola iliidhinishwa baada ya majaribio kadhaa kuonesha imewasaidia wagonjwa mahututi wa COVID 19 kupata nafuu.

Marekani ina wagonjwa milioni 1.1 wa virusi vya corona na kurekodi vifo 65,000 hali inayomfanya rais Donald Trump kuwa mbioni kubadili hali wakati taifa hilo lilio na uchumi mkubwa duniani likirekodi idadi kubwa ya watu waliokosa ajira kutokana na janga la virusi hivyo.

The post Marekani yaidhinisha dawa ya dharura kwa wagonjwa wa virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.