Manchester United inapigiwa upatu kumnyakua winga wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore, hata hivyo United itachuana na Liverpool na Manchester City katika mbio za kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Birmingham Mail)

Man Utd 'join Liverpool, Man City and Bayern' in Adama Traore ...

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19 alikataa mpango wa kuhamia Juventus mwezi Januari kwa kuwa timu hiyo ilikuwa na mpango wa kumjumuisha katika kikosi cha wachezaji wa umri wa chini ya miaka 23. (La Repubblica, via Star)

Mshambuliaji wa Manchester City Leroy Sane hana mpango wa kuhamia kwa mahasimu wao katika ligi ya primia, Liverpool. Mchezaji huyo, 24 raia wa Ujerumani anaendelea kujiandaa kuhamia Bayern Munich. (Bild, via Sports Illustrated)Leroy SaneLeroy Sane

Arsenal wana matumaini ya kumsajili winga anayechezea kikosi cha wachezaji wa umri wa chini ya miaka 21, katika klabu ya Bayer Leverkusen Moussa Diaby. Kinda huyo, mwenye 20 ambaye ni mchezaji wa zamani wa Paris St-Germain alitengeneza magoli mawili katika ushindi wa Leverkusen dhidi ya Werder Bremen siku ya Jumatatu. (Le 10Sport-in French)

Chelsea wanaongoza katika mbio za usajili wa beki wa kati wa kiholanzi Xavier Mbuyamba, 18, kutoka kwa miamba ya Uhispania Barcelona, hayo ni kwa mujibu wa wakala wa kinda huyo. (Voetbal International, via Mail)Xavier MbuyambaXavier Mbuyamba

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Newcastle United Danny Rose, 29, anaamini Mauricio Pochettino- Kocha wake wa zamani katika klabu ya Tottenham Hotspur- ipo siku ataifundisha Manchester United. (The Lockdown Tavtics, via Team Talk)

Klabu kadhaa za Ulaya zinamnyemelea beki wa Spurs Jan Vertonghen, ambaye anamaliza mkataba wake msimu huu. Mchezaji huyo mwenye miaka 33 na raia wa Ubelgiji amepewa ofa za usajili na Real Betis ya Uhispania, pia vilabu vya Italia, Inter Milan na Roma wanamtolea macho mchezaji huyo. (Star)Jan VertonghenJan Vertonghen

Kiungo wa Manchester United James Garner, 19 ataruhusiwa kuondoka kwa mkopo msimu ujao, wakati ambapo vilabu vya Cardiff City, Swansea City na Sheffield Wednesday wakiwa na nia ya kumchukua muingereza huyo. (Mail)

The post Man United yapimana ubavu na Liver, City kumsajili Adama Traore, kinda wa miaka 19 agoma kujiunga na Juventus appeared first on Bongo5.com.