Mwanamke mmoja nchini Argentina ameiandikia barua mamlaka ya nchi yake kumsaidia kumuachia huru muuaji wa mtoto wake kwa sababu anaumwa pumu hivyo gerezani ni sehemu hatari kwake.

Silvia Ontivero aliwasiliana na mahakama mapema mwezi Februari ,akilalamikia ombi la muuaji wa kijana wake kutoka gerezani.

Hata hivyo , jinsi hali ilivyo sasa amefikiria tena.

“Nilikuwa na kinyongo. Nilikuwa na chuki . Lakini sikuwahi kutamani afe, aliandika kwenye barua yake.

Siku ya Jumanne, rais wa Argentina, Alberto Fern√°ndez aliweka mpango wa kuwalinda wafungwa kwa kuwaamisha kuwapeleka katika nyumba watafungiwa wakiwa salama wawezavyo.

Kumekuwa na ghasia katika magereza katika nchi yote wiki za hivi karibuni, wakilalamikia kuwa virusi vya corona vitaweza kusambaa kwa haraka katika mkusanyiko wa watu ambao hakuna usafi.

Maamuzi ya rais yalisababisha watu washindwe kuelewa wengine wakihofia haki inaweza isitendeke wakati wengine wakisisitiza kuwa kuwaachia huru kutasababisha maambukizi zaidi kuenea.Wafungwa walizua ghasia katika jela ya Villa Devoto mjini Bueno Aires baada ya kisa cha kwanza cha Covid-19 kugunduliwa

Mtoto wa Silvia Ontivero, Alejo Hunau, aliuliwa katika mji wa Andean huko Mendoza mwaka 2004.

Diego Arduino alihukumiwa kifungo cha miaka 16 kutokana na uhalifu aliofanya.

Jumanne ilikuwa siku ya kusikiliza kesi hiyo, Jaji Mariana Gardey alisema Arduino alikuwa miongoni mwa wafungwa 400 katika magereza ya Mendoza kuwa katika hatari ya kuathirika kiafya kutokana na hali zao.

Katika barua ya wazi iliyoandikwa na bi.Ontivero alisema ilimuwia vigumu kufikiria suala la kufungiwa nyumbani, lakini amekuja kuunga mkono wazo hilo.

“Tulikuwa tunazungumzia kitu tofauti hapa. Mlipuko. Kuna msongamano wa watu wengi gerezani na ninavuta taswira hofu ambayo wako nayo wakiwa ndani,” aliandika.

Alikiambia pia chombo cha habari cha TN news kuwa kumuacha muuaji huyo gerezani , itakuwa sawa na hukumu ya kifo, kitu ambacho nilikuwa nakipinga siku zote.

Bi. Ontivero alikuwa mwanasiasa wa magereza kwa miaka saba wakati taifa hilo likiongozwa kwa utawala wa kimabavu, mwaka 1976 mpaka 1983.

Awali alisema kuwa kifungo kilikuwa kinampa muda Arduino kutafakari na kubadilika mtu mwema, ndio maana alipinga ombi la awali.

Mtoto wake alikuwa mwandishi wa habari na mshauri wa serikali ya Mendoza

Aliuwawa akiwa nyumbani kwake, akiwa anakunywa mvinyo.

Jumatatu, ghasia za kuvunja gereza la Peruvian mji mkuu wa Lima, lna kusababisha watu tisa kuuwawa.

Mmlaka ya gereza ilisema kuwa wafungwa walikuwa wanahamasishana kuvunja gereza baada ya wafungwa wawili kufariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kamishina mkuu wa UN Human Rights Michelle Bachelet, aliyekuwa rais wa Chile, ametaka magereza kufanyiwa usafi na wafungwa ambao si hatari sana kuachiwa huru.

Jinsi chanjo ya corona itakavyofanya kazi

Maelfu ya wafungwa kutoka Chile na Colombia waliachiwa huru katika kipindi hiki cha mlipuko.

Wiki iliyopita seneta wa Mexico’s aliruhusu hatua hizohizo kuchukuliwa.

Hatahivyo El Salvador, alidai kuwa wahalifu hao wanatumia fursa ya mlipuko huu ili kujinufaisha wao.

Jumatano, kulikuwa na uamuzi ambao ulikuwa haujaeleweka Argentina, baada ya Carlos Capdevila, daktari ambaye alihukumiwa kwa kosa la kuwa na utu kuwa miongoni mwa watu ambao walipewa nafasi ya kupelekwa kwenye ‘kifungo cha nyumbani’.

Jaji alisema , mfungwa huyo mwenye miaka 70- alikuwa anafanya kazi katika kituo maarufu cha kushikilia wahalifu cha Esma wakati wa utawala wa kimabavu, alikuwa katika hatari ya kupata virusi vya corona kwa sababu ya hali yake ya kupata presha ya juu na kansa ni hatari zaidi.

The post Mama aandika barua kuomba muuaji wa mtoto wake kutolewa gerezani   appeared first on Bongo5.com.