Madereva 19 wa Malori wa Tanzania waliotajwa kukutwa na Virusi vya Corona nchini Kenya, wamepimwa tena hapa nchini na Vipimo vyao kuonyesha hawana maambukizi ya Virusi hivyo.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, leo Mei 20, 2020, imesema Mkoa huo umejiridhisha kuwa hatua hiyo ni mbinu ya kuua Sekta ya Utalii katika Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kuanzia Mei 14 mwaka huu, Mkoa huo ulianzisha utaratibu wa kuwapima Madereva wanaotoka nchini Kenya, ambapo hadi Mei 16 Madereva 24 walikutwa na Virusi vya Corona, ambapo 20 kati yao ni Wakenya.

The post Madereva Watanzania waliodaiwa kuwa na corona Kenya, wapimwa Tanzania na kukutwa hawana appeared first on Bongo5.com.