Madereva 25 kutoka Tanzania wamezuiwa kuingia nchini Kenya baada ya kukutwa na virusi vya corona. Kati ya madereva hao 23 ni raia wa Tanzania , mmoja wa Uganda na mmoja kutoka taifa la Rwanda.

Kulingana na wizara ya afya nchini Kenya madereva hao walipimwa na kupatiwa matokeo yao katika kipindi cha saa 24 kwenye mpaka wa Namanga.

Serikali ya Kenya imesema kwamba hatua ya kuzuia madareva hao kuingia nchini humo inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya maambukizi kutoka kwa raia wa kigeni.

Katika mkutano wake na wanahabari katibu tawala wa waziri wa Afya Rashid Aman aliongezea kwamba maabara mbili za kuhama hama zitazinduliwa katika mpaka wa Namanga ili kuimarisha upimaji wa wagonjwa wapya.

 

Aman aidha amewataka Wakenya wanaoishi mipakani kuwaripoti watu wanaowashuku ambao wanajaribu kuingia nchini kwa njia haramu.

Wakati huohuo naibu huyo amesema kwamba wagonjwa wapya 22 wameripotiwa nchini Kenya na hivyobasi kuongeza idadi ya wagonjwa wa Covid-19, kufikia 737.

Idadi hiyo ni kati ya sampuli 1,516 zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Amesema kwamba kufikia sasa serikali ya kenya imefanikiwa kuwapima watu 35, 432 .

Madareva wa malori ya masafa marefu wakizubiri kupimwa Covid-19 katika mpaka wa MalabaMadareva wa malori ya masafa marefu wakizubiri kupimwa Covid-19 katika mpaka wa Malaba

21 kati ya wagonjwa hao ni Wakenya huku mmoja akiwa raia wa Uganda

Waziri huyo hata hivyo alitangaza kwamba wagonjwa wanne walifariki kutokana na virusi hivyo, watatu kutoka Nairobi na mmoja kutoka Mombasa.

Hatua hiyo inaongeza idadi ya waliofariki kutokana na Covid-19 kufikia watu 40. Wagonjwa wapya ni watu wenye umri kati ya 20 hadi miaka 81.

Kati ya wagonjwa hao wapya , 10 wanatoka Nairobi , wanane kutoka Mombasa , watatu kutoka Kajiado na mmoja kutoka Bomet.

Mgonjwa wa hivi karibuni wa Bomet inafanya idadi ya kaunti zilizoathirika na ugonjwa huo kufikia 20.

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Wagonjwa walioripotiwa Nairobi wanatoka; Embakasi (4), Kamukunji (3), Kibra (2) na KNH (1).

Mjini Mombasa, wagonjwa saba wanatoka Mvita huku mmoja akitoka Nyali.

The post Madereva 25 kutoka Tanzania wazuiliwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na Corona appeared first on Bongo5.com.