Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 21 2020 anawaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.Viongozi wanaoapishwa ni

1. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake Wazee na Watoto.

2. Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

3. Dkt. Jacob Gideon Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria

4. Balozi Mteule Phaustine Martin Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji

5. Balozi Mteule John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya

6. Brig. Gen. John Julius Mbungo kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU.

Hafla inayofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.