Amerika Kusini ina baadhi ya magereza yaliyofurika watu duniani. Yakiwa na wafungwa waliobanana ndani ya vyumba vidogo vya mahabusu -kimoja kikiwa na watu 12 agizo la kutosogeleana haliwezekani na huduma duni za matibabu zinamaanisha kuwa mlipuko wowote wa virusi vya corona unaweza kusambaa kama moto wa nyikani.
Umoja wa mataifa umezitaka serikali kuweka mikakati ya kuwalinda wafungwa na umependekeza wale wenye uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya corona waachiliwe kwa muda ili kupunguza kujaa kwa magereza kupita kiasi.
Chile, Colombia na Nicaragua zimetangaza kuwa zitawahamishia maelfu ya wafungwa katika kifungo cha nyumbani kipaumbele kikipewa wazee, wanawake wajawazito na wenye magonjwa ya kudumu.
Brazil tayari imeanza kuwahamisha wafungwa zaidi ya 60 katika kifungo cha nyumbani mahabusu na Peru inasema inapanga kuwapa msamaha wafungwa wenye uwezekano mkubwa wa kuuambukizwa corona.
Lakini nchi yenye idadi ya pili kwa wingi wa wafungwa baada ya Marekani bado haijachukua hatua zozote.
El Salvador imekua ikikabiliwa na tatizo la magenge ya wahalifu kwa miongo kadhaa na wafungwa wake ni wengi kupita kiasi.

Ilimchukua mpigapicha Tariq Zaidi miaka miwili kupata picha za hali katika jela za El Salvador kabla ya mlipuko wa virusi vya corona katika taifa hilo la kati la Amerika. Alifanikiwa kuingia katika magereza sita pamoja na mahabusu mbuili za polisi katika fursa ya nadra ndani ya taasisi hizo za kisheria.

Licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafungwa ikilinganishwa na idadi ya watu kwa ujumla, El Salvador ni moja ya nchi zenye viwango vya juu vya mauaji katika nchi moja duniani.
Lakini kiwango hicho kimekua cha chini kutoka kiwango cha watu 17.6 kwa siku mwaka 2015 hadi wastani wa 3.6 wa mauaji vilivyoripotiwa Oktoba 2019 na halafu tena wastani wa vifo 2.1 mwezi machi 2020.
Rais Nayib Bukele, ambaye aliingia madarakani Juni 2019, anadai kuwa ndiye aliyewezesha kushuka kwa viwango hivyo vya mauaji.
Sera yake ya kutovumilia kabisa magenge ya wahalifu pia inatekelezwa katka magereza ya nchi ambapo wafuasi wa magenge hawaruhusiwe kutembelewa na wageni wala kumiliki simu na huzuiliwa ndani ya mahabusu kwa saa 24 kila siku. Na pale, hali ndani na nje ya jela inapokua ya utulivu haki za kutembelewa hurejesha tena.

Kabla Bwana Bukele aingie madarakani, mpango ulioitwa “Yo cambio” (Ninabadilika ) uliwapatia wafungwa fursa ya kujifunza kazi ambazo zingeinua uwezo wao wa kupata ajira.


Baadhi hata walibuni mitindo yao na kuionyesha katika maonyesho ya fasheni ya magereza.

kutokana na tatizo kubwa la magenge na ukweli kwamba hadi 80% ya mashambulio hutekelezwa nje i yanaaminiwa kuwa huwa yameagizwa kutoka ndani ya magereza, wengi wanahofia kwamba kuwaachilia wafungwa kutaongeza ghasia za magenge ya wahalifu.

Walinzi wa magereza mara nyingi huvaa barakoa zinazofunika sehemu kubwa ya nyuso zao na shingo ili kuficha utambulisho wao ili kujilinda na familia zao zisilengwe

Lakini magereza yaliyofurika wafungwa yanaweza pia kuwa vitovu vya maambukizi ya virusi vya corona.
Magonjwa ya mfumo wa kupumua tayari ni mengi katika magereza ya nchi. Kiwango cha maradhi ya kifua kikuu(TB) katika magereza ya El Salvador yamekua ni zaidi ya mara 50 kuliko yalivyo katika idadi nzima ya wakazi wa nchi hiyo, kwa mujibu wa jarida la – Pan American Journal of Public Health Study.
Kutokana na kwamba virusi vya corona na kifua kikuu husambaa kwa njia sawa, maafisa wanang’ang’ana kujiandaa kwa kile mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi Jorge Panameño amekiita “bomu linalosubiri muda” kulipuka.

Rais Bukele amekua akifanya mabadiliko katika mfumo wa magereza wa El Salvado . Tarehe 26 Disema -kabla ya virusi vya corona havijasambaa nchini El Salvador – alitangaza kwamba gereza la Chalatenango (katika picha ya juu) litabadilishwa na kuwa chuo kikuu.
Wafungwa mia sita walihamishwa na rais alisema kupitia Twitter bila kutoa maelezo zaidi-kwamba wafungwa 730 waliobaki watahamishwa siku zinazofuatia.
Lakini japo rais Bukele aliharakisha kutoa amri ya kukaa nyumbani kote nchini na ya kutotoka nje ili kukabiliana na virusi, hakuna sera rasmi ya kuwaachilia wafungwa ambayo imetangazwa.
Magereza ya El Salvador yana uwezo wa kuwahifadhi wafungwa 18,051 lakini kwa sasa yanawafungwa zaidi ya 38,000.
Joto kali, hali za mbaya za uchafu na kifua kikuu vimegharimu maisha ya wafungwa wengi hata kabla ya virusi vya corona.

Janga la virusi vya corona limeleta tatizo kubwa kwa rais Bukele.
Kujianda kwa uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya corona magerezani, rais tayari ameondoa baadhi ya hatua za dharura alizoweka za kuwadhibiti wafungwa.

Zaidi ya hayo, Majaji nchini El Salvador wametaka wafungwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na wenye magonjwa yasiyopona waachiliwe kwa muda -hata hivyo wafuasi wa magenge hawatajumuishwa katika hatua hii.

Anakabiliwa na suala moja gumu: kuwaachilia wafungwa na hatari katika ghasia za magenge ya wahalifu ambayo amepambana kuyapunguza au kuwaweka ndani ya magereza na kukabiliwa na uwezekano wa mlipuko wa virusi vya corona.
Chanzo BBC
The post Lifahamu gereza lenye msongamano mkubwa wa wafungwa, Chumba kimoja watu 12 appeared first on Bongo5.com.