Msanii wa filamu na muziki, Kitale ameonyesha nyumba yake mpya ambayo alikuwa anaijenga Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mchekeshaji huyo huyo ameandika ujumbe huu baada ya kuonyesha mjengo huo. “Hii nyumba nimeaanza kuijenga 201, kisa Cha kununua kiwanja maeneo Ya Kigamboni tulienda kushoot filamu yangu, wakati tunaendelea na Shooting pembeni pakawa na minong’ono ya wenyeji wetu kwamba kuna kiwanja Kinauzwa. Pesa Sina ila Nina gari (NOAH)….. nikawapigia Madalali wa Kuuza na Kununua magari SINZA nikawaambia nauza gari Kwa Bei sawa na bure akaniambia Tuma picha nikawatumia wakaipenda gari, wakaniuliza gari ipo wapi ?? Kuna Mtu anaitaka …nikaawambia nipo location Kigamboni Kama Masihara Majama wakaja na Pesa.

Nikawauzia gari nikanunua kiwanja Palepale tukarudi kwa Pikipiki Kambini.* Mwaka mzima Nikaanza kuweka Matofali Mwaka ulivyopinduka nikajikuta Nina tofali elfu 5 Baada ya Hapo ujenzi ndio ukaanza Rasm na ndio leo Hii ndio tumefikia hapo.

Ashukuliwe M/Mungu kwa Kwa vikwazo vyote nilivyopitia kipindi najenga Kiasi Kwamba nilitaka kukata tamaa lakini M/Mungu alikuwa pamoja na Mm kwa kila Hatua. 💪💪 Hakuna Kukata Tamaa …Kwa Kauli fasaha Nyumba Ni ya Mkude Simba na Mwanae Bwakila, Msije Mkasema Nyumba Ya Kitale …Kitale anadaiwa na Mkude Simba Hadi leo ajalipa deni.” KITALE

The post Kitale aonyesha mjengo wake wa mamilioni, atoa funzo jinsi alivyoujenga (Video) appeared first on Bongo5.com.