Polisi Kaunti ya Nakuru nchini Kenya, wameanzisha uchunguzi baada ya jamaa mmoja kujisalimisha mwenyewe akidai kumuua jirani yake ambaye anadaiwa kufanya mapenzi na mke wake.

 

Mshukiwa aliyetambuliwa kama Julius Kiplagat, mwenye miaka 31, alikiri kumuua Kipkemboi Tomno baada ya kutambua kwamba ana mahusiano ya kimapenzi na mke wake.

Mshukiwa huyo wa mauaji anadaiwa kwenda nyumbani kwa marehemu Kipkemboi siku ya Jumamosi na kumuua kwa madai ya kutembea na mkewe.

Kulingana na ripoti ya polisi, Kiplagat alisema kuwa alifanya uchunguzi na kugundua kuwa mke wake ana mahusiano ya kimapenzi na jirani yake. “Alisema alifanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya mke wake kuwa katika mahusiano na marehemu, na ana uhakika kuwa jirani amekuwa akitembea na mke wake,” ilisoma ripoti hiyo.

Mshukiwa huyo wa mauaji anadaiwa kwenda nyumbani kwa Kipkemboi siku ya Jumamosi, Mei 9 na kumshambuliwa kwa panga na kisha kuingia katika Kituo cha Polisi cha Menengai West na kukiri kufanya mauaji hayo. Mwili wa mwathiriwa ulipekwa katika hifadhi ya maiti ya Kaunti ya Nakuru huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi.

Source Nairobi News

The post Kisa mke afanya mauaji kwa jirani yake na kujipeleka polisi, Kenya appeared first on Bongo5.com.