Kweli kipaji unacho kijana..leo unakwama wapi. Kwenye maisha usifanye maamuzi ukiwa na hasira au furaha sana. Ona sasa wale jamaa zako waliokuambia jamaa hakufai anakuharibia ANAKUNYONYA. Ona sasa walisema anakunyonya umeona show ya fiesta unavyolipwa..ona wasivyokuwa hata busy na wewe tena. Leo huna hata hit songs upo upo tu mzee. Kijana siyo kila ushauri unachukua..

Mavoko ni kama mimi

1. Mwaka 2016 kuna rafiki yangu wa karibu alikuwa ananishauri nimuache demu wangu kwamba hajatulia..jamaa akadai kamuona maisha club akiwa na wana wengine mara kibao....Nikafata ushauri ..nikapiga demu chini demu alilia sana.. February, 2017 jamaa huyo huyo kamuoa demu aliyenishauri nimuache. Leo nina miaka 30 naokota mizoga tu sina mtoto wa maana. Siyo kila ushauri wa kufata. Na wamepata mtoto mmoja wanaishi Tegeta Nyuki. Leo naumia nilimuacha bank teller yule kiboya sana.

2. Nilimaliza chuo Mzumbe 2011 first degree, nikapata kazi ya muda jhpiego iliyopo pale karibu na victoria njia ya bagamoyo road. Mm nilikuwa research officer.. sasa jamaa wale walitupromise watatupa ajira within six months..sasa mpka mwaka ukaisha hakuna ajira ya kudumu. Ninaye anko wangu mmoja akaniambia ukimaliza mkataba wako wa mwaka 1 acha kazi chukua mafao yako ( gratuity) tukafanye biashara ya Ruby..aisee hakuna kipindi nilipata pressure km ile. Nikawa napigiwa mchoro wa kununua ruby na kuuza najiona km utajiri kesho tu..daah. Millioni 12 zangu zote mafao na saving zilivyoisha kwenye biashara ya ukichaa ya madini..Maisha haya basi tu. Wale jamaa zangu leo wameajiwa wote na waliongeza wengine.


Siyo kila ushauri wa kuchukua.

Kuna mwana mmoja anaishi Tabata anastudio juzi kaniambia Mavoko anastress sana wadau wake wote walimshika masikio wamemkimbia. Hata dada ake DOKII KAMKAUSHIA..WATANZANIA HAWAMINIKI. Mavoko alikuwa anaelekea kimataifa leo hata ndani hayupo mainstream.Sasa Hivi hata demu wale lulu diva hataki kumsikia mavoko.

WANASEMA BORA KIDOGO CHA UHAKIKA KULIKO KIKUBWA AMBACHO HUKIJUI.
Tumshirikishe Mungu kwenye kila ushauri tunaopewa na tuishirikishe sana akili zetu. Hisia ukifata utapotea.

Pole Mavoko. Kutake risk ni vyema but kwakutumia Akili.