Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amejitokeza hadharani baada ya kutokuonekana kwa siku 20 na kumaliza uvumi ulioenea kuwa amefariki dunia.

Mbali na kusemekana amefariki dunia pia ilidaiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuwa kiongozi huyo wa taifa la Korea Kaskazini amefanyiwa Operesheni ya Kichwa.

Kiongozi huyo alionekana akikata utepe mwekundu wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha mbolea huko Sunchon, vyombo vya habari vya serikali viliripoti, na kutoa picha zinazodaiwa kuonyesha tukio hilo.

Kim alionekana akitabasamu na kuzungumza na wasaidizi wake katika sherehe hiyo, lakini uhalisi wa picha hizo haukuweza kuthibitishwa kama kweli yupo hai.

 

 

The post Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Ajitokeza hadharani appeared first on Bongo5.com.