Manchester United wanataka kumsaini kiungo mahiri wa Argentina Thiago Almada, 19, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, kutoka Velez Sarsfield. (Tutto Mercato Web, via Express)
Mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil, 31, hataondoka klabu hiyo msimu huu na badala yake atakamilisha mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake na Gunners . (Fanatik, via Football London)
Arsenal wanamatumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 23, kwa mkopo hadi msimu wa sasa wa ligi ya primia utakapo kamilika, lakini wanapanga kurefusha mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania katika klabu hiyo kwa msimu mwingine. (El Confidencial, via Metro)
RB Leipzig wameungana na Everton katika kinyang’anyiro cha kumsaka beki wa Ufaransa wa miaka 20- Jean-Clair Todibo kutoka Barcelona. (HITC)
Manchester United bado hawajakubaliana kuhusu mkataba mpya na kiungo wa kati Angel Gomes,19, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa Juni. (Goal)
Mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius analengwa na Manchester United, kiungo huyo raia wa Brazil aliye na miaka 25 anaweza kununuliwa na klabu nyingine ikiwa italipa £88m kabla ya kuanza majadiliano ya mkataba. (Sun)
Winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, anasema Liverpool walitaka kumsajili kabla ya ajiunge na Manchester City kutoka Leicester City lakini Reds walisitisha mpango huo walipompata Mohamed Salah kutoka Roma. (Bein Sports, via Manchester Evening News)
Chelsea wana amini watampata Charlie Webster, ambaye anaripotiwa kunyatiwa na Borussia Dortmund, katika mkataba wa wa kitaalamu atakapofikisha miaka 17 Januari ijayo. (Telegraph)
The post Kinda wa miaka 19 kutoka Argentina kutua Man United kwa kazi maalum, Mesut Ozil yupo sana Arsenal appeared first on Bongo5.com.