Marekani imetangaza vikwazo kwa raia wa kigeni kuingia nchini humo wakitokea nchini Brazil, nchi ambayo kwa sasa inaendelea kuandikisha idadi kubwa ya mamabukizi ya Corona.

Watu ambao wamekuwa nchini Brazil kwa siku 14 zilizopita, kwa sasa hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani, baada ya taifa hilo la America Kusini kuwa taifa la pili duniani kuripoti visa vingi vya mamabukizi ya Corona

Hadi sasa Brazil imeripoti visa 360,000 vya corona huku watu wengine zaidi ya 22,000 wakipoteza maisha.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema masharti hayo yatasaidia kupambana na virusi vya Corona nchini Marekani kwa kuzuia mamabukizi mapya kuingizwa nchini humo.

Masharti haya yanawalenga zaidi raia wa nchi zingine ambao wamekuwa Brazil kwa siku 24 zilizopita na walikuwa wameomba kibali cha kuingia nchini Marekani.

Hata hivyo, masharti hayo hayaathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili.