Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameshangazwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa  Dar es salaam Paul Makonda kuwataka wakazi wa mkoa huo kucheza Disco kama sehemu ya shukrani kwa Mungu

Kupitia ujumbe wake aliotuma kwenye mtandao wa Twitter Lema amesema kitendo hicho kinaweza kuleta adhabu kuu

“Mungu atakuwa disco gani kwa hapo Dar ?Dhihaka zenu zinanuka adhabu kuu” ameandika Lema

Lema ametoa kauli hiyo ikiwa ni masaa machache tangu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwataka wananchi wa mkoa huo kutumia siku ya jumapili kushukuru Mungu kwa kusherekea