Kamati Kuu ya CHADEMA leo May 09,2020 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa,Freeman Mbowe, imeanza vikao vyake vya ki-digitali (CHADEMA Digital), vikao vitajadili agenda mbalimbali ikiwemo hali ya corona na Siasa nchini na kufikia maazimio ambayo yatatolewa kwa umma baada ya vikao kukamilika.

Kufanyika kwa kwa vikao vya Kamati Kuu CHADEMA vilivyoanza leo kwa njia ya mtandao, tunatekeleza kwa vitendo, ushauri ambao Chama kimekuwa kikitoa kwa Serikali na Bunge katika kuchukua tahadhari ya kupunguza mikusanyiko katika kuendesha shughuli zake,ili kujikinga na corona”-Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano’-CHADEMA